here

Monday, August 21, 2017

Zijue Sababu za Wanandoa Wengi Kuchepuka

Kwa karne hii katika mahusiano mengi  ya kimapenzi, ukiaachana na suala zima la ugonjwa wa ukimwi kwa sasa limeingia gonjwa jipya, na gonjwa hili limesbabisha maisha ya wengi kuingia matatatani. Na gonjwa hili si jingine bali ni gonjwa la kuchepuka. Gonjwa hili ilimesababisha mahusiano mengi kuingia matatani na si matatani tu bali wakati mwingine limepelekea mahusiano mengi kufa kabisa.

Na miongoni mwa sababu ambazo zinazochangia watu wengi kuchepuka ni kama ifuatavyo:

1: Kutoridhishwa katika tendo la ndoa
Kumekuwepo na malalamiko mengi na yatofauti baina ya wanandoa wanaume na wanawake katika suala hili. Wanaume wanalalamika kwamba wake zao mara baada ya kuolewa na hususani wakishapata watoto wanaanza kuwa wazembe na wasiojituma kwenye tendo la ndoa kama walivyokuwa awali.

Tafiti zinaonyesha kwamba mara mwanaume anapohisi kutoridhishwa kwenye tendo la ndoa ananafasi kubwa zaidi ya kutoka nje mapema kuliko mke wake. Wanawake wanauvumulivu wa ziada na kwa wale waliotoka nje ya ndoa zao walifanya hivyo baada ya uvumilivu wa miaka mingi na kukosa tumaini.

Kutoridhishwa katika tendo la ndoa kunaweza pia kusababishwa na maumbile ya mwili, kwa mfano watu wenye miili mikubwa na uzito mkubwa hupata shida kwenye kuwaridhisha wenzao ukizingatia kwamba tendo la ndoa ni zoezi la kimwili “physical exercise”. Mtu wa jinsi hii anaweza kushindwa kwasababu ya ukubwa wamwili, kushindwa kuutuma mwili wake kadri anavyotaka na pia wengine kuishiwa pumzi au kuchoka mapema na hivyo kufika kileleni mapema sana. Hali hii husababisha kutoridhika kwa wanawake wengi sana kwenye ndoa.

2. Penzi kupoa au kufa
Penzi linapopoa au hata linapokufa huwa hali huwa inaonyesha wazi kabisa. Kwenye kupoa mhusika anaweza kuanza kujihisi ndani ya moyo wake kutompenda mwenzake kama alivyokuwa akimpenda awali. Inawezekana mwenzake hajagundua kuanzia mwanzoni kwamba penzi la mpenzi wake limepoa ila kama hali ya kupoa huku itaendelea lazima itagundulika.

Baadhi ya vitu dhahiri vitakavyoweza kukufanya ufahamu kwamba penzi la mwenzako limepoa au kufa ni kwamba kuna mambo ambayo uliyazoea kuyaona yakifanywa kawaida hautayaona tena. Kuna vitu vilikuwa vikifanywa pasipo kukumbushana sasa utalazimika kuviomba ili ufanyiwe, utaona kila kitu kinakuwa kigumu kumhusu mwenzako na hata uongeaji au kujibu kwake kunakuwa na walakini.

3. Ushawishi wa marafiki
Wako watu wengi sana kwenye ushauri wa wanandoa na hata wale wasiowanandoa ambao wamekiri kuchepuka kwasababu ya kushawishiwa na marafiki. Ni lazima ukafahamu nguvu waliyonayo marafiki. Usipokuwa na hekima ya juu ya kuweza kuchagua nani wa kuwanaye rafiki na nani sio basi utajikuta unapelekeshwa kila upande hata kule usipopenda utapelekwa kwasababu tu nguvu ya maamuzi haiko kwako tena bali iko kwa marafiki zako.

Yamkini unasema mimi ni rafiki tu sifanyi vile wanavyovifanya wao, mimi nasikiliza na kuchangia tu hoja zao, lakini ngoja nikwambie, taratibu utasikiliza, taratibu utaanza kuchangia na taratibu utavutika kuyafanya yale wanayoyafanya.

Yamkini wao kuchepuka ni hadithi ya kwaida na kwako sio kawaida, ukiendelea kukaa nao kidogokidogo utaanza kuona kuchepuka sio kitu cha kushangaza sana maana wengine nao wanafanya, na utaanza kidogokidogo na mwisho utakuwa mtaalamu. Wako waliofundishwa kiutaniutani leo hii ni wataalamu kuliko walimu wao. Jifunze kuwa na msimamo, Jifunze kuchagua marafiki wanaokujenga na sio kukubomoa. Jifunze kufanya maamuzi binafsi yenye busara na yasiyokufungulia milango ya majuto.

Hizo ni mingoni mwa sababu chache kati ya nyingi ambazo husababisha watu wengi kuchepuka. Siku ya kesho tuitaangalia namna ya kuachana mchepuko na kubaki njia kuu.

No comments:

Post a Comment