here

Monday, August 21, 2017

‘Wanasiasa chanzo cha Bombadier kukamatwa’

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (Maelezo), Zamaradi Kawawa

BAADHI ya wanasiasa nchini wametajwa kutengeneza mgogoro wa utekelezaji wa ununuzi wa ndege ya tatu kutoka kampuni ya Bombadier ya nchini Canada kwa kuweka maslahi yao binafsi na ya kisiasa mbele badala ya maslahi ya Taifa.

Pamoja na juhudi hizo za wanasiasa hao kutaka kukwamisha ununuzi wa ndege hiyo, Serikali kupitia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (Maelezo), Zamaradi Kawawa  imesema kwamba hatua za kidiplomasia na za kisheria zinachukuliwa ili kumaliza jambo hilo na ndege hiyo itawasili wakati wowote nchini.

Kaimu Msemaji huyo wa Serikali alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa taarifa ya wanasiasa hao inadai kwamba kuna wanasheria wa kampuni fulani ya nchini Italia wameweka zuio la la ununuzi wa ndege hiyo kwa madai kwamba wanakamata mali hiyo kwa kuwa kuna kampuni inayoidai Serikali ya Tanzania.

Kwa mujibu wa Kawawa, wanasheria waliofungua madai kwamba Serikali inadaiwa na kwamba ndege hiyo ishikiliwe hawana uhalali wowote wa kufanya hivyo na ni matapeli ambao wamesukumwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wasioitakia mema Tanzania.

“Kwa kuwa Serikali ilishapata fununu kwamba kuna baadhi ya viongozi wa chama cha siasa wana mpango huo, sasa watu hao wamejidhihirisha hadharani kwamba wao ndio wako nyuma ya pazia la kuhujumu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa maslahi yao,” alisema Kawawa na kuongeza: “Serikali ya Awamu ya Tano inawahakikishia Watanzania kwamba ndege itakuja.

Wanaokwamisha jitihada za serikali za kuleta ndege watapanda, na ndugu zao watapanda, na wafuasi wao watapanda pia.” Aliongeza kuwa mbali na kutaka kuhujumu juhudi za ununuzi wa ndege hiyo, kundi hilo la baadhi ya viongozi wa siasa wameshawahi kushawishi wafadhili wasilete misaada tena Tanzania na kuwaomba washirika wa maendeleo pia wasilete misaada nchini.

Alisema kuwa Serikali imesikitishwa kwa hujuma zinazofanywa waziwazi tena kwa ushabiki na baadhi ya viongozi wa kisiasa wa chama hicho kupinga jitihada za Rais za kuliletea taifa maendeleo.

Alieleza kuwa mbali na kuhujumu jitihada za maendeleo, watu hao pia wanahujumu hali ya usalama wa raia kwenye baadhi ya maeneo nchini. Licha ya nia ya wanasiasa hao kuwashawishi wafadhili na wadau wa maendeleo kuacha kuisaidia Tanzania, Kaimu Msemaji huyu wa Serikali alisema kwamba washirika wa maendeleo wameongeza kasi ya ushirikiano na serikali ya Rais John Magufuli.

“Serikali ya Marekani kupitia Balozi wake hivi karibuni imesema itaongeza kiasi cha misaada Tanzania. Bill Gates pia ameonesha kuguswa na kasi ya uongozi ya Rais Magufuli na kuahidi kutoa fedha zaidi, lakini pia viongozi wakuu wa nchi 15 wamekuja nchini tangu Rais Magufuli aingie madarakani,”alieleza Kawawa.

Serikali kupitia Kaimu Msemaji Mkuu huyo imesema kwamba imekuwa ni hulka kwa baadhi ya viongozi wa siasa kubeza jitihada za dhati za Rais Magufuli za kuwaletea wananchi maendeleo ikiwemo kunusuru madini na maliasili, kusimamia uadilifu, uaminifu na uwajibikaji katika suala zima la makinikia hali iliyomfanya Rais wa Kampuni ya Barick kuja nchini kumuona Rais Magufuli.

Kawawa alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haibagui Watanzania kwa itikadi za kisiasa, dini, kabila, rangi au utofauti wowote. Alisema kwa mtu yeyote mwenye uchungu na nchi yake angepambana kwa jambo linalohusu maslahi ya Taifa likiwemo la kununua ndege ili lisikwame badala ya kushabikia

No comments:

Post a Comment