here

Tuesday, July 25, 2017

WAZIRI MENO MAKALI

Waziri Ummy Mwalimu amsimamisha kazi mganga mfawidhi Mlandizi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Waziri Ummy Mwalimu amemsamamisha kazi mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi Stanley Mpola kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Waziri Ummy alitoa agizo hilo jana alipokuwa tembelea kituo hicho cha afya kabla ya kukabidhi magari matatu ya kubebea wagonjwa, mawili yakiwa yametolewa na Mbunge wa kibaha vijijini Mh. Amoud Jumaa na moja likiwa ni ahadi ya Mh. Rais John Magufuli.

Akiwa katika kituo hicho waziri huyo  alipewa malalamiko kutoka kwa mama mmoja Salma Halfan aliyedai alifanyiwa upasuaji katika kituo hicho na alitozwa gharama ya vifaa vya  upasuaji kiasi cha shilingi laki 180,000.

Hata hivyo mganga huyo alimweleza waziri kuwa fedha hizo hazikutolewa katika kituo hicho bali mgonjwa huyo alipewa orodha ya vifaa akaenda kununua mwenyewe kwenye duka la dawa.

Hata hivyo Waziri Ummy alisema gharama za vifaa hivyo ni kubwa kulinganisha na hali halisi ya upasuaji huku akiwa watupia lawama watumishi wa afya kuwa hata maduka ya dawa wanayoelekeza wagonjwa wamiliki wake ni wao wenyewe.

" Tunajigamba huduma kwa wanawake wanaokwenda kujifungua ni bure, alafu nyie mnawachaji wanawake wajawazito, hii orodha mliyompa ni kweli vifaa vyoyote hivi hakuna, na hizi gloves 17 ni za nini alizonunua, ni kweli zinatumika zote? Hamna hata huruma, wanawake wajawazito mmewafanya mtaji, kuna haja gani ya kuja katika kituo cha afya wakati gharama zinazidi zile za hospitali binafsi," alisema Waziri Ummy.

Waziri huyo aliagiza apate orodha ya wauguzi wote waliokuwa zamu siku hiyo na waliomuhudumia mgonjwa huyo ili waweze kuchukuliwa hatua .

"Orodha yote ya waliohusika kumuhudumia mgonjwa huyu niipate kesho, nitarudi tena kuongea na watumishi, na huyu mama naagiza ahamishiwe hospitali ya rufaa Tumbi kwa usalama wake, mnaweza mkafanya lolote amekuwa jasiri kunieleza kero yake, na ole wake mtumishi wa afya atakayemfanyia kitendo kibaya mjamzito naahidi kula naye sahani moja", alisema Ummy.

Alisema ilani ya uchaguzi ni pamoja na matibabu bure kwa wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano na wazeee wasiojiweza hivyo serikali kwa kuhakikisha inatekeleza ilani yake haitamvumilia mtumishi yeyote wa afya atayeshindwa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.

"Siwezi kukubali hata mara moja kuona watumishi wa afya wanaocheza na afya za wananchi wetu na kitu ambacho nataka watanznaia wanikumbuke ni pamoja na kuboresha afya za wajawazito, natoa salamu kwa waganga wote katika halmashauri na mikoa nchi nzima watoe huduma bora za afya hasa afya ya mama na mtoto, na ndio kipaumbele changu, alisema Waziri wa Afya

No comments:

Post a Comment