here

Wednesday, July 26, 2017

Usishangae ukimuona Zlatan Man United, sababu ya Lukaku kusajiliwa kwa dau kubwa

Kocha wa Man United Jose Mourinho ameripotiwa na mtandao wa dailymail kuonesha dalili za wazi kuwa Zlatan Ibrahimovic anaweza kurudi Man United na kusaini mkataba mpya, Man United hawakumuongezea mkataba mpya Zlatan wenye thamani ya pound 367,640 kwa wiki baada ya kuumia.
Zlatan baada ya kuumia mwezi April atakuwa nje ya uwanja hadi 2018 lakini Mourinhoameonesha viashiria vya kuwa kuna uwezekano wa Zlatan kurudi Man United wakati akizungumzia ishu ya kumsajili Romelu Lukaku kwa dau la pound milioni 75 dau ambalo ni kubwa.
“Tumetumia pesa nyingi kwa ajili ya mshambuliaji kwa sababu ya aina ya mshambuliaji tuliyekuwa tunamtaka na tumetumia kwa sababu ya kilichotokea kwa Zlatan hatuwezi kuruhusu kukaa miezi sita ya msimu bila kuwa na mshambuliaji mahiri” >>> Mourinho
Kauli ya Jose Mourinho inaashiria kuwa Zlatan ambaye kwa sasa anatumia bado miundombinu ya Man United kuponesha jeraha lake la goti anaweza kurudi Man Unitedbaada ya kupona 2018 licha ya kuwa namba yake ya jezi namba 9 amepewa Lukaku.
VIDEO: Gor Mahia vs Everton: Full Time 1-2 (ALL GOALS JULY 13, 2017)

No comments:

Post a Comment